Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto awakaribisha walinzi wake wapya nyumbani kwake, wanywa chai pamoja

4efc8a04ca4d3442 Ruto awakaribisha walinzi wake wapya nyumbani kwake, wanywa chai pamoja

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amewakaribisha maafisa wapya wa ulinzi nyumbani kwake mtaani Karen. Ruto amefanya mkutano na walinzi hao kabla ya kunywa chai pamoja nao. Maafisa hao wa kitengo cha utawala watakuwa wakimlinda Ruto nyumbani kwake baada ya wale wa kitengo cha GSU kuondolewa na serikali. Naibu Rais William Ruto amefanya mkutano na maafisa wapya wa ulinzi kutoka kitengo cha utawala ambao amepewa na serikali.

Kwenye video ambazo amepakia mitandaoni, Ruto anaonekana akiwa matembezini na maafisa hao katika boma lake kabla ya kuketi chini kunywa chai pamoja nao.

" Nanywa chai na walinzi wangu wapya, nawakaribisha katika makazi yangu rasmi," Ruto alisema.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, serikali ilimpokonywa Ruto walinzi ambao walikuwa maafisa wa kitengo cha GSU waliokuwa wakilinda makazi yake yalioko mtani Karen na yale ya Sugoi.

Maafisa hao waliondolewa siku ya Alhamis, Agosti 26, hatua iliyomfanya Ruto kulalamikia usalama wake.

Msemaji wa naibu Rais William Ruto Davidi Mugonyi alisema mabadiliko hayo yalifanywa bila mazungumzo wala makubaliano yoyote.



Mugoyi alisema kamanda wa polisi mtaani Karen alipata amri kutoka afisi kuu ikimuagiza kuwaondoa maafisa hao haraka kabla ya majira adhuhuri.

Ruto pia amedai kwamba wapinzani wake wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanakamdamiza kabisa kisiasa.

Awali, mfanyakazi wake mkuu Ken Osinde alikuwa amelalama kwamba walinzi wa Ruto walikuwa wamepunguzwa bila serikali kutoa taarifa yoyote.

Maafisa hao waliondolewa wakati ambapo tofauti baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake zimeonekana hadharani hali ambayo imemfanya rais kumtaka naibu wake kujiuzulu kama amechoka.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke