Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto awaangukia wakulima

Rais Wa Kenya William Ruto Ruto awaangukia wakulima

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya William Ruto amewaomba wakulima nchini humo kuongeza juhudi shambani ili kusaidia kupunguza hali ngumu ya maisha na bei za vyakula.

Akizungumza katika Kanisa la African Inland Church (AIC), mjini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu wakati wa ibada ya Jumapili Aprili 9, Ruto amesema anafahamu ukweli kwamba Wakenya wengi wanateseka kutokana na gharama ya juu ya maisha na bei ya vyakula.

Ameongeza kuwa serikali yake inafanya kila iwezalo kubadili hali hiyo akibainisha kuwa kuanzia wiki ijayo bei zitashuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live