Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto atoa maagizo mazito kwa polisi kukomesha mauaji

Ruto Atoa Maagizo Mazito Kwa Polisi Kukomesha Mauaji Ruto atoa maagizo mazito kwa polisi kukomesha mauaji

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Kenya William Ruto amesisitiza dhamira ya serikali yake kukomesha mauaji ya kiholela nchini humo, kwa kuagiza shirika la polisi kuandaa mipango ya mageuzi na uangalizi wa raia.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kusambaratisha kitengo cha polisi kinachodaiwa kuhusika na mauaji na watu kutoweka ambao wameongezeka katika miaka ya hivi majuzi.

Ripoti zinasema kuwa hatua hiyo ilifuatia uchunguzi wa kutoweka kwa raia wawili wa India na dereva wao wa eneo hilo mwezi Julai.

Polisi wa Kenya walikuwa wameangaziwa wiki hii iliyopita kuhusu mauaji ya mwanahabari wa Pakistani Ashrad Sharif katika kile wanachodai kuwa ni kisa cha utambulisho kimakosa.

Mauaji hayo hapo awali yamesababisha dhoruba ya kidiplomasia, huku serikali zikitaka haki kwa raia wao waliouawa. Wiki iliyopita, maafisa 12 wa polisi wa Kenya waliambiwa watakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa madai ya kuhusika katika makosa yaliyofanywa wakati wa uchaguzi wa 2017, ikiwa ni pamoja na mauaji ya mtoto wa miezi sita.

Chanzo: Bbc