Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto ataka tathmini nyongeza ya mishahara

Mahakama Kenya Yakataa Ombi La Rais Ruto Kuhusu Kodi Ruto ataka tathmini nyongeza ya mishahara

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya Dk. William Ruto ameiagiza Ofisi ya Hazina kuangalia upya tangazo la nyongeza ya mishahara akitaka maafisa wote wa mihimili kuendelea kuishi kulingana na uwezo wao.

Taarifa ya Ruto imesema tathmini hiyo ni sharti ikazingatia maamuzi ya kuondolewa kwa Mswada wa Sheria ya Fedha wa 2024 na matazamio ya vikwazo vya fedha “Hii maana yake hali itakuwa tofauti na awali, hivyo watendaji wanapaswa kuishi kulingana na uwezo wao.”

Nyongeza ya mishahara ilianza kutumika Julai 1. Mshahara huo mpya uliochapishwa kwenye gazeti la serikali unahusu mishahara na marupurupu ya maafisa wa Serikali katika Utendaji wa Serikali Kuu, Seneti, Bunge, serikali za kaunti na tume huru.

Wakati mishahara ya Rais na naibu wake imetajwa kuendelea kama ilivyokuwa, Mishahara ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri na Mawaziri wengine itaongezeka hadi Shilingi za Kenya 990,000 kutoka Sh957,000.

Makatibu Wakuu, Mkaguzi Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa sasa watapokea Sh819,844 kutoka Sh792,519 kwa mwezi.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai atapata Sh684,233 kutoka Sh652,742 hapo awali. Maspika wa Bunge na Seneti watapokea Sh1,208,362 kila mwezi kutoka Sh1,185,327 kila mmoja.

Manaibu Spika sasa watapokea Sh966,690 kila mwezi, huku viongozi wa Wengi na walio wachache wakipokea Sh800,019. Wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti pia watachukua Sh739,600 kama mshahara wa jumla, kutoka Sh725,502.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live