Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto ashinda alikopigia kura Martha Karua

Ruto Wachina Kenya Ruto ashinda alikopigia kura Martha Karua

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika jana yameonyesha katika kituo alichopigia kura mgombea mwenza wa urais, Martha Karua wa Azimio la Umoja, Naibu Rais William Rutto amepata kura nyingi kuliko mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga

Karua alipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Mugumo kilichopo katika jimbo Gichugu ambapo Ruto amepata kura 911 na Odinga amepata kura 311.

Kushindwa kwa Odinga katika kituo hicho kunatoa ishara mbaya kwa Odinga, Karua na timu yao ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.

Matokeo ya kituo hicho yaliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya kupitia fomu 34A  yameonyesha Ruto kuongoza hali iliyosababisha baadhi ya wafuasi wa mwanasiasa huyo kushangilia. Mwisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live