Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto ashauriwa kuwa na mfumo wa kudhititi wageni wanaoingia Kenya bila visa

Ruto Un Baraza Yusalama Ruto ashauriwa kuwa na mfumo wa kudhititi wageni wanaoingia Kenya bila visa

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Voa

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia ya kimataifa wamesema sera ya Rais wa kenya William Ruto ya kuruhusu raia wa kigeni kuingia nchini humo bila visa itahitaji kuwepo kwa mifumo thabiti ya uhamiaji inayolenga kudhibiti uhalifu wa aina yoyote katika mipaka yake.

Wakizungumzia kuhusu utekelezaji wa sera hiyo ya kuwaondolea visa raia wa nchi mbalimbali duniani wanaoingia Kenya, Profesa Chacha Nyaigoti Chacha mfuatiliaji wa diplomasia ya kimataifa aliiambia Sauti ya Amerika kuwa serikali ya rais Ruto inajaribu kuwavutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Profesa Chacha alikuwa akitoa maoni kufuatia hotuba ya Rais Ruto ambaye aliwaambia wakenya katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, kuwa wasafiri wote wa nchi za kigeni kuanzia Januari mosi mwaka ujao watahitaji tu idhini ya kusafiri ya kieletroniki kuingia nchini humo.

Hata hivyo, Profesa Chacha anaeleza kuwa mahusiano ya kidiplomasia ya nipe nikupe huiwezesha nchi kujiendeleza kwa misingi ya mahusiano yaliopo kati ya nchi mbili na kukosekana kwake kunaweza kuwa mzigo kwa nchi inayoondoa mahitaji ya visa.

Ingawa mahitaji ya visa yameondolewa, kwa mujibu wa masharti mapya ambayo serikali ya Kenya imeyachapisha hivi majuzi, imeweka utaratibu mpya wa usafiri ikiwa ni kwamba wageni wanaoingia Kenya, kuanzia Januari mosi mwaka ujao watahitajika kupata idhini ya kielektroniki ya kuingia Kenya itakayogharimu dola thelathini za Kimarekani.

Kupitia mfumo huo wa kidigitali, serikali itakuwa na lengo la kuhakikisha kwamba wasafiri wote wanaoingia Kenya wanatambuliwa mapema kwenye mfumo wa kielektroniki kabla ya kusafiri.

Wakati wa maadhimisho hayo ya uhuru wa Kenya, Rais Ruto aliwaambia wakenya kuwa serikali yake imelazimika kufanya maamuzi magumu, kwa kuweka kando utekelezaji wa mipango muhimu ya maendeleo na badala yake kuwekeza katika mifumo anayosema imeiondolea nchi dhoruba na msukosuko wa kiuchumi.

Akitafakari hatua ambazo Kenya imepiga katika kipindi cha miongo sita iliyopita, Ruto anasema nchi kama Singapore, Malaysia na Korea Kusini zilizo na umri sawa na ule wa Kenya yamekomaa na yamepiga hatua kubwa zaidi za kiuchumi na yamestawi, ishara kuwa Kenya inahitaji maendeleo ya kiasi kikubwa. Hasa kwa ujenzi wa maelfu ya nyumba na kubuni kazi, hatua anayoimithilisha na ufanisi wa Singapore, Malaysia na Korea Kusini anazosema zimetekeleza miradi kama hiyo kwa kipindi cha miaka 40 na kustawi kwa kiwango hicho.

Chanzo: Voa