Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto asema muungano wa Kenyatta na Raila uliua ajenda nne za Jubilee

4c1e147497a94efe Ruto asema muungano wa Kenyatta na Raila uliua ajenda nne za Jubilee

Sat, 20 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto ameendeleza mashambulizi yake dhidi ya kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga, akimlaumu kwa kulemaza utawala wa Jubilee.

Naibu Ruto amesema salamu za maridhino baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Odinga yaliua ajenda Nne Kuu za serikali na anasema yuko tayari kutimiza agenda hizo iwapo atachaguliwa kuwa Rais mwaka ujao.

DP pia alimkashifu bosi wake Rais Kenyatta kwa kumuunga mkono kiongozi wa ODM kuwania urais kabla ya uchaguzi wa 2022 licha ya kwamba alikuwa adui yao w kisiasa.

DP Ruto alisema salamu za maridhiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Odinga ziliua ajenda Nne Kuu za serikali, ambazo sasa anasema yuko tayari kuzifufua iwapo atachaguliwa kuomgoza nchi 2022.

DP pia alimkashifu bosi wake Rais Kenyatta kwa kumuunga mkono kiongozi wa ODM kuwania urais kabla ya uchaguzi wa 2022 licha ya kwamba ni mtu wa nje ya Jubilee.

Akizungumza huko Kiritiri, Kaunti ya Embu, Ijumaa, Ruto alimshutumu rais kwa kuwapuuza wafuasi waliojitolea wa Jubilee na kuwapendelea adui wake wa zamani na mpinzani wao mkuu katika uchaguzi uliopita.

"Unaniambia kwamba sisi sote, milioni nane, tumeunda serikali mara mbili, kwamba hakuna hata mmoja wetu anayeweza kutuongoza?" Ruto alisema.

“Kweli? Hapana. Je! hilo si tusi kubwa? Je, hilo si tusi? Kwamba miongoni mwetu sote, watu milioni nane, hatuwezi kupata mtu ambaye anaweza kutuongoza na kwamba wanapaswa kuajiri mtu mwingine?”

Ruto alidai Odinga alitikisa mashua ya chama tawala cha Jubilee, na hivyo basi kukwamisha ajenda kuu nne za serikali na miradi yake yote.

Alipuuzilia mbali msukumo wa Rais Kenyatta na Odinga wa kurekebisha Katiba badala ya kuendeleza ajenda Nne Kuu ambazo alisema zilinuiwa kuinua maisha ya Wakenya.

DP Ruto, katika ziara yake ya pili katika Kaunti ya Embu, aliahidi kutenga pesa za serikali zitakazotumika kama ruzuku kwa biashara ndogo ndogo iwapo atachaguliwa kuwa Ikulu.

Alisema utawala wake utapa kipaumbele uchumi, akiongeza kuwa mtindo wake wa chini kwenda juu utakuwa jibu la mapambano yanayowakabili Wakenya.

Naibu Rais aliahidi kuendelea na miradi yote ambayo utawala wa Rais Kenyatta haujaweza kutimiza na ambayo waliahidi kwa Wakenya wakati wa kampeni zao za 2017.

Ruto alisema akichaguliwa "atafufua" ajenda Nne Kuu na kuwekeza Ksh.100 bilioni ndani yake ili kubuni nafasi za kazi, kuhakikisha usalama wa chakula, kuanzisha huduma za afya kwa wote na kufufua viwanda.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke