Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto asaini muswada afya kwa wote

Kenya: Ruto Afanya Mabadiliko Katika Baraza La Mawaziri Ruto asaini muswada afya kwa wote

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Kenya, rais wa Kenya William Ruto Alhamis ya wiki hii, amesaini kuwa sheria miswada minne itakayofanikisha mpango wa afya kwa wote ambapo wafanyakazi wote watachangia asilimia 2.75 ya mishahara yao kufadhili mpango huo.

Rais Ruto, amesema mfuko huo utahakikisha wakenya wote wanapata huduma za afya, ambapo wafanyikazi wote watachangia mfuko huo utakaochukua nafasi ya bima ya afya ya NHIF ambapo wakenya wamekuwa wakichangia kati ya shilingi 150 hadi 1700 kutibiwa katika hospitali za uma na binafsi.

Waziri wa afya Susan Nakhumicha, akipigia upatu mpango huo, amesema ni bora zaidi kwakuwa hautawabagua wakenya kwa msingi wa mapato yao.

Hata hivyo wakenya wengi wameupinga baadhi wakiutazama kama ushuru mpya ambao ni wa juu, ukilinganisha na hali ngumu ya maisha kwa sasa.

Mashirika ya kiraia pamoja wa wanaharakati wa huduma bora za afya pia wameukosoa mpango huo wanaosema hautaweza kukidhi mahitaji yote ya afya kutokana na mfumuko wa bei ambao umeathiri sekta zote

Chanzo: www.tanzaniaweb.live