Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto apendekeza mrithi wa Gachagua

WhatsAppImage2024 10 17at22.jpeg Ruto apendekeza mrithi wa Gachagua

Fri, 18 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Kithure Kindiki amependekezwa kuchukua wadhifa wa Naibu Rais hatua inayokuja baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua na Bunge la Seneti.

Rigathi Gachagua alitimuliwa jana jioni kufuatia utaratibu ambao haujawahi kushuhudiwa na kumaliza kilele cha mzozo wa miezi kadhaa kati ya Rais William Ruto na Naibu wake.

Rigathi Gachagua, mwenye umri wa miaka 59, anayeshutumiwa kwa ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka, anakuwa Naibu wa kwanza wa Rais kuondolewa Mamlakani.

Mchakato huu wa kihistoria unaibua sintofahamu nchini Kenya, ikizingatiwa kuwa demokrasia thabiti katika eneo lisilo na utulivu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live