Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto aongoza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru nchini Kenya

Ruto Anapeleka Nchi Katika Mwelekeo Ufaao Wahome Thuku Akiri(1) Ruto aongoza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru nchini Kenya

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Kenya William Ruto, ameongoza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru nchini Kenya.

Sherere hizo ambazo zimeandaliwa katika uwanja wa Uhuru jijini Nairobi zinahusisha hafla muhimu ya kuzindua kikosi cha jeshi la nchi kavu ambalo litafahamika kama 25 Mechanised Infantry Battalion.

Hiki ni kikosi cha tano katika brigedi ya nane ya jeshi la nchi kavu.

Ni cha pili kukabidhiwa bendera rasmi na Rais William Ruto ambaye mwaka jana alikipatia kikosi cha 23MIB bendera yao ya kuhudumu. Baada ya kukabidhiwa bendera iliyoombewa na wakuu wa dini ....bendera hiyo ilionyeshwa katika maonyesho rasmi yanayofahamika kama ‘Trooping of the colors’ ambapo wanajeshi walioandaa gwaride maalum wanashiriki katika mipangilio maalum yaani military formations uwanjani.

Rangi za kikosi kipya ni Maroon ambayo pia itakuwa rangi rasmi ya kikosi hicho cha 25 MIB.

Bendera hiyo ni muhimu sana na hulindwa vikali kwa maana ndio ishara muhimu ya uhuru wa kazi wa kikosi husika. Na inapopepea ina maana kwamba kikosi kiko kazini na huongozwa na afisa mkuu jeshini.

Katika miaka ya hivi maajuzi ...jeshi la nchi kavu limekuwa likifanya mabadiliko ya kutumia silaha za kisasa vitani na kubadili vikosi vyake kutoka Kenya Armed Rifles hadi Mechanised Infantry Batallions ambazo zinatumia magari aina ya personel carrier's yaani APC katika shughuli zao za kivita.

Katika miaka ya hapo awali...jeshi la nchi kavu limebuni brigedi ya nane ambayo ina vikosi yaani battalions za ,23,25 MIB huku Rais wa awali Uhuru Kenyatta akizindua pia vikosi vya 17,19 na 21 Kenya Rifles.

Hafla ya Trooping of the Color huandaliwa kila mwaka katika sherehe za Jamhuri na ni tamaduni ambayo Kenya imeiga kutoka kwa jeshi la Uingereza ambalo lilikuwa linasimamia taifa hilo wakati wa ukoloni.

Ni hafla ambayo hufanyika katika uwanja wa kambi za kijeshi ama za kitaifa kama ule wa Uhuru ambapo amiri jeshi mkuu wa majeshi husimamia sherehe hizo.

Bendera huonyeshwa na kikosi husika ambapo piano wanajeshi hufanya maonyesho rasmi ya kuonyesha bendera hiyo.

Chanzo: Bbc