Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto aomba radhi vifo vya watu walioangamia Shakahola

Kiongozi Wa Kenya Aomba Radhi Kwa Vifo Vya Watu Walioangamia Shakahola Ruto aomba radhi vifo vya watu walioangamia Shakahola

Mon, 15 May 2023 Chanzo: Bbc

Rais William Ruto amewaomba Wakenya msamaha kutokana na vifo vya Wakristo walioangamia katika kanisa la kufunga hadi ufe, akikiri ulegevu na kuridhika kutoka kwa upande wa serikali.

Zaidi ya miili 200 hadi sasa imetolewa katika msitu wa pwani wa Shakahola, ambapo waumini walilazimika kufa kwa njaa ili kukutana na Yesu. Zaidi ya watu 600 bado hawajulikani walipo.

"Ninachukua jukumu kwamba, kama rais, haya (mauaji ya Shakahola) hayakupaswa kutokea. Kwa hilo, nasema kweli, samahani," Bw Ruto alisema katika mahojiano ya televisheni na vyombo vya habari vya Kenya Jumapili.

Aliwalaumu polisi na maafisa wa ujasusi nchini kwa kushindwa kugundua shughuli za ibada hiyo kwa wakati.

Alisema maafisa husika watalazimika kutoa maelezo kuhusu mauaji hayo ya halaiki.

Rais alisema kwamba atafanya kila awezalo kuzuia vifo vya kidini siku zijazo.

Pia aliahidi kutembelea msitu wa Shakahola mara uchunguzi utakapokamilika.

Chanzo: Bbc