Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto amuonya Odinga juu ya wimbi jipya la maandamano

Rais Ruto Apata Pigo, Aambiwa Nyadhfa 50 Za Mawaziri Si Halali Ruto amuonya Odinga juu ya wimbi jipya la maandamano

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Rais William Ruto ameapa kuwa maandamano dhidi ya serikali ya siku tatu mfululizo yaliyotangazwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wiki ijayo, kuwa hayatafanyika na kumuonya kiongozi huyo wa Muungano wa Azimio Raila Odinga atakabiliana naye.

“Uchaguzi umekwisha. Huwezi kutafuta uongozi kwa kutumia damu ya Wakenya na kuharibu mali yao,” amesema akiwa mjini Naivasha.

“Demu hizi hayatatokea. Nisikilize kwa makini: Huwezi kutumia njia zisizo za kisheria, zisizo za kikatiba kutafuta mamlaka nchini Kenya. Subiri 2027. Nitakushinda tena.”

Pia alitangaza kuwa hakutakuwa na “handshake” akisema hiyo ilimaliza Kenya.

“Nitasimama imara. Sitatikisika hata kidogo. Kenya ni yetu sote. Sio ya maandamano,” alisema mkuu huyo wa nchi.

"Unaweza kufanya maandamano nyumbani kwako tu, sio mahali pengine popote. Fanya mambo haya yote unayotaka kufanya nyumbani kwako, sio mahali pengine popote. Hatuwezi kukubali hilo.”

Awali, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, alitangaza kuwa maandamano dhidi ya serikali yatafanyika kwa siku tatu mfululizo wiki ijayo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.

Muungano huo ulisema hatua hiyo imetokana na matakwa ya umma, na kupitia tena mpango wake wa awali ambao ulikuwa umesema kuwa maandamano, yatafanyika siku ya Jumatano pekee.

Chanzo: Bbc