Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto amuombea Rais Uhuru, amuomba Mungu abariki serikali ya Jubilee

B3a62d11c7901d20 Ruto amuombea Rais Uhuru, amuomba Mungu abariki serikali ya Jubilee

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu wa Rais aliandaa kikao hicho cha maombi nyumbani kwake Karen mnamo Jumanne, Septemba 7Wakati wa kikao hicho cha maombi, Ruto aliwaidhinisha Seneta wa Murang'a, Irungu Kang'ata na wakili Edward Muriu Rais Uhuru Kenyatta na Ruto walitofautiana tangu handisheki ya Machi 9, 2018, kati ya kiongozi wa taifa na hasimu wake kisiasa Raila Odinga Video ya Naibu Rais William Ruto akimuombea bosi wake Rais Uhuru Kenyatta imesambaa, licha ya wawili hao kupigana vita baridi.

Naibu wa Rais aliandaa kikao hicho cha maombi nyumbani kwake Karen mnamo Jumanne, Septemba 7, alipofanya mkutano wa mashauriano na viongozi kutoka Gatanga, kaunti ya Murang'a.

Wakati wa kikao hicho cha maombi, Ruto aliwaidhinisha Seneta wa Murang'a, Irungu Kang'ata na wakili Edward Muriu.

''Tunamleta rais mbele zako na sisi sote tunaohudumu chini yake na uongozi mzima wa taifa hili ili Mungu aweze kutusaidia kupata ufanisi na kutambua upendo wako kwa taifa letu," aliomba Ruto.



Ruto pia alimuomba Mungu kusaidia taifa hili kukabiliana na changamoto kadhaa ikiwemo janga la COVID-19.

''Pia tunaombea changamoto zinazotukabili kama taifa kama vile janga la COVID-19 ili uweze kutupa maarifa na hekima ya kupambana nalo vyema ili kufungua uchumi wetu na tuendelee kukuabudu makanisani," aliomba Ruto.

Ruto aombea umoja KenyaPia aliombea umoja miongoni mwa Wakenya akimuomba Mungu kuisaidia taifa kukabiliana na ukabila na umaskini.

"Tusaidie kama taifa tuweke pamoja kama taifa la Kenya. Tuondolee umaskini na ukabila. na utufanye ili mipango yetu yote yafaulu kulingana na mapenzi yako. Tuko na chakula mbele yetu tunaomba Mwenyezi Mungu ukibariki na uwakumbuke ambao hawana chakula kwa njia yako ya kipekee uweze kuwapa...Tunaomba kwa ajili ya hawa viongozi wengine wote. Amina," aliomba

Rais Uhuru Kenyatta na Ruto walitofautiana tangu handisheki ya Machi 9, 2018, kati ya kiongozi wa taifa na hasimu wake kisiasa Raila Odinga.

Maridhiano hayo ndio yanadaiwa kuwa chanzo cha mpasuko kati ya Uhuru na Ruto.



Tuju amsuta RutoKatika kile kilidhihirisha kifo cha Chama cha Jubilee, katibu mkuu Raphael Tuju mnamo Jumatatu, Septemba alimsuta Ruto akimshtumu kumhujumu Uhuru.

Tuju, alikosoa namna Ruto aliweza kupata mali yake na kumtaka kuanika kiasi cha pesa analipa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Ushuru (KRA) kutoka kwa faida yake ya KSh 1.5 milioni anazopata kwa biashara yake ya kuuza mayai.

Uhuru amtaka Ruto ajiuzuluHaya yanajiri wiki mbili baada ya Rais Uhuru kumtaka naibu wake Ruto ajiuzulu.

Uhuru alimtupia Naibu Rais William Ruto makombora na kupanua mpasuko kati ya viongozi hao wawili ambao walianza kutofautiana baada ya chaguzi za mwaka 2017.

Katika mahojiano na waandishi wa habari katika Ikulu Jumatatu, Agosti 23, Uhuru akisemekana kukerwa alisema iwapo Ruto hafurahishwi na serikali anavyodai, anatakiwa ajiuzulu na kupeleka ajenda yake kwa watu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke