Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto amuita Raila "Mradi wa Serikali" kwenye uchaguzi wa 2022

54e0a92d47d08298 Ruto amuita Raila "Mradi wa Serikali" kwenye uchaguzi wa 2022

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ruto anasema Raila ni mradi wa serikali ambao umeletwa kwa Wakenya ili wameze kama dawa. Amesema atawaongoza wafuasi wake kuhakikisha kuwa wamemshinda Raila ifikapo 2022 ili astaafu pamoja na Rais.

Akipiga kampeni kule kaunti ya Lamu alisema yuko tayari kumenyana na Raila na kumpa funzo la kisiasa 2022Naibu Rais William Ruto amepuuza kampeni za kinara wa ODM Raila Odinga kuingia Ikulu 2022 akisema yeye ni project.

Akipiga kampeni kule kaunti ya Lamu alisema yuko tayari kumenyana na Raila na kumpa funzo la kisiasa 2022.

Aliwataka wafuasi wa Jubilee kuingia UDA akisema sasa wameletewa aliyekuwa mpinzani wao 2013 na 2017.

Alisema Raila ni mradi wa watu fulani ambao walisambaratisha Jubilee na sasa wanataka Raila aingie Ikulu kurithi Rais Uhuru Kenyatta.

"Hatuwezi watu milioni nane tuliosimama kidete mpaka tukaunda serikali ati kwa sababu wamevunja chama ya Jubilee sasa watulazimishe tukatafute mgombea wa kukodisha akuje awe mgombea wetu," Ruto alisema.

Alisema yuko tayari kukabiliana na Raila na kuahidi wafuasi wake kuwa kuna karata ambazo atawachezea.

"Hio haiwezekani, mtakubali kuletewa project? Na msijali na hawa wanatusumbua, hawa wanatusumbua tutawashinda. Mnajua wamejaribu kunipangia, lakini mimi pia nimewapangia," alisema DP

Kilio cha Ruto kinajiri wakati ambapo Raila anaonekana kuwa na uhusiano mzuri na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na serikali yake huku DP akitengwa.



Kuna ripoti kuwa Raila sasa ndiye chaguo la Rais Uhuru kuchukua mamlaka ifikapo 2022 ili kumrithi.

Mjadala kuhusu uwezekano wa Raila kuungwa mkono na Rais ulianzishwa na naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe.

Murathe aliashiria kuwa uchanganuzi wake unamwambia Uhuru atamuunga mkono Raila katika kile alisema ni 'Raila moment'.

Kubadilika kwa siasa tangu handisheki ilipofanyika kumekuwa changamoto kubwa kwa DP Ruto na wandani wake ambao wamekuwa wakiendesha kampeni za kuingia Ikulu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke