Rais wa kenya William Ruto amesema yuko tayari kukutana ana kwa ana kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ‘’wakati wowote’’.
Hii inakuja baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali ambayo yamezua taharukindani ya nchi hiyo na kimataifa.
"Kama unavyojua siku zote ninapatikana kukutana na wewe ana kwa ana kwa urahisi’’, Ruto alisema kwenye chapisho akimfahamisha Raila Odinga kupitia ukurasa wa Twitter uliobadilishwa kwa jina la X.
Awali, Bw Odinga aliwaambia waandishi wa habari wa kimataifa kuwa Rais Ruto alimualika Rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwapatanisha ili kurejesha hali ya utulivu, lakini Rais Ruto hakujitokeza kushiriki mazungumzo hayo.
Odinga alisitisha maandamano mwezi Aprili na Mei baada ya Ruto kukubali mazungumzo, lakini mazungumzo hayo yalivunjika, na baadaye Muungano wa Azimio uliandaa duru kadhaa za maandamano mwezi huu, yaliyobadilika kuwa ghasia.