Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto amteua CDF mpya

Charles Kahariri Ruto amteua CDF mpya

Thu, 2 May 2024 Chanzo: Bbc

Rais William Ruto wa Kenya amempandisha cheo Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini humo Luteni Jenerali Charles Kahariri kuwa Jenerali wa 11 wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo.

Jenerali Kahariri anashika wadhifa huo kufuatia kifo cha Jenerali Francis Ogolla kilichotokea mwezi Aprili mwaka huu katika ajali ya helikopta huko Elgeyo Marakwet.

Rais Ruto pia amempandisha cheo Meja Jenerali John Omenda kuwa Luteni Jenerali na kuwa Makamu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya.

Mabadiliko mengine ameyafanya kwenye baadhi ya Kamandi za Jeshi la Ulinzi la Kenya ambapo Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed ameteuliwa kuwa Kamanda wa Jeshi la Anga.

Chanzo: Bbc