RAIS William Ruto ameipongeza Rwanda kwa mchango wake katika ujumbe wa amani Mashariki mwa DR Congo.
Ruto amesema Rais Paul Kagame ametoa uongozi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaolenga kuhakikisha kuna amani ya kudumu katika nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki.
"Ninataka kupongeza uelewa wa Kagame na Rwanda kuhusu masuala ya Mashariki mwa DRC na kwa EAC tunapodhibiti hali hiyo," Ruto alisema Jumanne akiwa Rwanda.
"...Amewahakikishia watu wa DRC ambao wamekuwa na changamoto kwa miaka mingi wanaweza kuwa na amani kwa mara nyingine na kujikita katika kujenga taifa lao."
Ruto amesema EAC inahitaji mchango mkubwa wa Rwanda katika kusaidia kushughulikia masuala yanayokabili mataifa jirani ya Ethiopia, Sudan na Sudan Kusini.
Mkuu huyo wa nchi ambaye yuko nchini Rwanda kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili alitumia fursa hiyo kutoa mwaliko wake kwa Kagame kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika utakaofanyika Nairobi.