Joho alidai kuwa Naibu wa Rais William Ruto anafanya mkutano wa kisiri na baadhi ya vinara wa NASA kubuni mrengo utakaotumika 2022Gavana huyo pia alisema yuko tayari kumuunga mkono atakayeteuliwa na ODM kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2022Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuwa atamchagua mrithi wake wa mwaka 2022 miongoni mwa vinara wa NASA
Gavana wa Mombasa Hassan Joho anadai kuwa Naibu wa Rais William Ruto anafanya mkutano wa kisiri na baadhi ya vinara wa muungano wa National Super Alliance (NASA) kubuni mrengo utakaotumika 2022.
Akizungumza na gazeti la Nation, Jumatatu, Juni 21, Joho ambaye ni mmoja wa wandani wa karibu wa kiongozi wa ODM Raila Odinga, alidokezea kuwa chama hicho kinafahamu njama hiyo ya baadhi ya vinara wa NASA kufanya mazungumzo na UDA.
"Wakati hawa watu wa NASA walikuwa wanabuni One Kenya Alliance na wakati Wiper ilikubaliana kuungana na Jubilee tulinyamaza hatukuwarushia mawe,"
"Hata sasa tunajua baadhi yao wanafanya mazungumzo na UDA lakini kama ODM hautujalalamika mbona wanataka kurudisha Kenya nyuma?" alimaka Joho.
Gavana huyo pia alisema yuko tayari kumuunga mkono atakayeteuliwa na ODM kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2022 akiwa na matumaini chaa hicho kitabuni serikali ijayo.
Kulingana na Joho, licha ya kulipa KSh1, milioni bado atamuunga mgombea yeyote atayechaguliwa na ODM hata asipochaguliwa.
Kauli ya Joho inakujia siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza kuwa atamchagua mrithi wake wa mwaka 2022 miongoni mwa vinara wa NASA endapo watakubaliana kumteua mgombea mmoja.
Kwa mara ya kwanza, Uhuru aliwataka vinara wa NASA kuungana pamoja ili kuhimarisha nafasi yao ya kubuni serikali mpya baada ya kukamilika kwa muhula wake 2022.
Haya pia yanakujia baada ya kiongozi wa Wiper na Mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi kukataa kumuunga mkono Raila kuwania urais 2022.
Raila naye kwa upande wake alisema alisema hamtegemei Uhuru kuingia Ikulu ila uamuzi wote unatokana na Wakenya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke