Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto akiri kumiliki helikopta na mashamba yanayolindwa na serikali

Abdb25659d5955d1 Ruto akiri kumiliki helikopta na mashamba yanayolindwa na serikali

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amemtaka waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i kufanyia viongozi wote 'Life style audit'.

Ruto amesema Matiang'i ni mtu mdogo serikalini lakini ameingiwa na kiburi na madharau licha ya kuwa yeye ndiye alimpa kazi.

DP amekiri kuwa anamiliki mali ambayo ilianikwa na Waziri Matiang'i wakati wa kuzungumzia usalama wake bungeniAlisema anakubaliana na asilimia 70 ya kilichowekwa wazi lakini amekanusha kumiliki shamba la ADC.

Akiongea Septemba 2 mtaani Karen alipokutana na wageni kutoka Nakuru, DP alikiri kumiliki mali ambayo ilitajwa na Matiang'i.

Amesema asilimia 70 ya mali hiyo ambayo ni pamoja na helikopta tano na mamia ya ekari ni matunda ya jasho lake.

"Hawa watu wa OP (afisi ya rais) walinisaidia kufanya life style audit, nilikuwa nimefanyiwa na amagazeti hapo awali lakini sasa wametoa ile haikuwa yangu kama hoteli ya 680. Walipata kama 70% hivi ni kweli," alisema DP.



Alitaja hatua ya Matiang'i kama lifestyle audit na kumtaka kuendelea na kuwafanyia viongozi wengine pia.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke