Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto akanusha taarifa ya kuwanyima chakula walinzi wake

5631e1e08cde96a1 Ruto akanusha taarifa ya kuwanyima chakula walinzi wake

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto ameyajibu madai kwamba maafisa wa utawala wanaolinda makao yake rasmi kwa wakati mwingine huwa hawapewi chakula.

Wizara hiyo ilisema maafisa hao huwa pale usiku na mchana na hukosa nafasi ya kuondoka na kwenda kutafuta chakula Msemaji wa DP Ruto David Mugonyi aliyakana madai kuwa, maafisa hao wanaolinda makao ya Ruto walinyimwa chakula au marupururupu ya chakula.

Wizara ya Masuala ya Ndani iliiomba ofisi ya Naibu Rais William Ruto kurudisha marupurupu ya mlo kwa maafisa wanaompa ulinzi.

Kupitia msemaji ya msemaji wake David Mugonyi, Ruto alisema sio kweli kwamba walinzi wake walikuwa wakinyimwa chakula au marupurupu ya chakula wakati wanapotekeleza majumu yao.

Hata hivyo, Mugonyi alipokuwa akizungumza na jarida la Daily Nation, alikiri kwamba marupurupu ya maafisa hao yalikuwa yamechelewa ila suala hilo linashughulikiwa.

“Tumekuwa tukiwapa chakula. Malalamishi niyayajua yanahusiana na kuchelewa kulipwa kwa kwa marupurupu yao. Maafisa hao wako chini ya Inspekta Jenerali wa Polisi. Maslahi yao huwa yanashughulikiwa na ofisi hiyo. Hata maafisa wa GSU wanasimamiwa na IG,” Mugonyi alijibu.

Mugonyi alikuwa akiyajibu malalamishi yalitolewa na Wizara ya Masuala ya Ndani kuhusu maslahi ya maafisa wa polisi tawala waliokuwa wakiyalinda makao rasmi ya Naibu Rais.

Katibu katika Wizara ya Masuala ya Ndani Wilson Njenga alikuwa alikuwa ameomba maafisa hao wapewe chakula ili waweze kutekeleza majumu yao ipasavyo. Alilalamika kwamba maafisa hao hawakuwa wakipewa marupurupu yao ya chakula kwa wakati unaofaa.

"Hii ni kukujulisha kuwa maafisa waliotajwa hawajakuwa wakipewa chakula au marupurupu ya chakula ili kuwawezesha kununua chakula na kuchapa kazi inavyohitajika. Huwa wako kazini kila wakati, usiku na mchana na hivyo hawawezi kutoka kutafuta chakula," sehemu ya barua hiyo ilisoma.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke