Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto agoma kusaini Mswada wa Sheria mpya ya Fedha

Ruto Kenya's Presdent Ruto agoma kusaini Mswada wa Sheria mpya ya Fedha

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, William Ruto, amekataa kusaini Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 ambao ulikuwa ukipingwa na Wakenya hali iliyopelekea vijana nchini humo wanaojiita 'Gen Z' kufanya maandamano.

Rais Ruto ameukataa Muswada huo uliopitishwa na Bunge jana kufuatia kupingwa na wananchi walioingia barabarani kwa maandamano tangu Juni 21, 2024.

Aidha, ikiwa Wabunge watafanyia kazi marekebisho hayo, Spika atalazimika kuurudisha kwa Rais lakini pia wanaweza kuupitisha tena bila Marekebisho ambapo upitishwaji wake utapaswa kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge nchini humo

Rais Ruto anahutubia Taifa muda huu ikiwa ni Hotuba ya pili baada ya nyingine aliyoitoa Juni 25, 2024 wakati kukiwa na Maandamano ya Vijana wanaopinga Muswada huo kupitishwa na Bunge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live