Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto afungua Bunge la Kifahari Kenya

Ruto Bunge As Ruto afungua Bunge la Kifahari Kenya

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya William Ruto leo Aprili 25, 2024 amefungua jengo la Bunge Towers lililo gharimu Ksh.9.6 bilioni baada ya kuahirishwa kwa uzinduzi huo wiki iliyopita.

Tarehe ya kwanza ya uzinduzi iliyopangwa Aprili 19 ilisogezwa mbele kufuatia kifo cha cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Francis Ogolla.

Jengo hilo la ghorofa 28 linakuja na seti ya huduma za kifahari za wabunge wa Kenya ikiwa ni pamoja na ukumbi wa mazoezi, chumba cha urembo na mgahawa. Pia, itakuwa na vyumba vya kamati ambapo wanachama watafanya biashara zao..

Wabunge watatarajiwa kulikalia jengo hilo kwa awamu mbili; Awamu ya kwanza itahusisha kuhamisha wanachama kutoka KICC hadi Mnara au malazi mengine mbadala, Awamu ya pili itakuwa na wabunge kutoka Continental House kukalia mnara huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live