Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto aafiki idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Ruto Un Baraza Yusalama Ruto aafiki idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Kenya William Ruto ameafiki idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kupelekwa kwa maafisa usalma wa Kenya Haiti

Baraza hilo lenye wanachama 15 siku ya Jumatatu lilipitisha azimio linaloidhinisha ujumbe wa 'Kikosi cha Usaidizi wa Usalama wa Kimataifa' unayoongozwa na Kenya kwa ajili ya kuwasaidia polisi wa Haiti katika kupambana na magenge ya uhalifu.

Azimio hilo lililoandaliwa na Marekani na Ecuador, liliidhinishwa kwa kura 13 za ndio huku China na Urusi zikijizuia kupiga kura.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne, Rais Ruto aliafiki a uamuzi wa baraza hilo, akiutaja kuwa " chombo muhimu cha kufafanua ujumbe wa kimataifa."

Ruto alielezea ujumbe huo kama wajibu wa kimaadili kwa jumuiya ya kimataifa.

"Hali ya Haiti ni suala la kuzingatia kibinadamu, uwajibikaji wa kimaadili na haki ya kimsingi, kwamba hatua zinapaswa kuongezwa kwa kiasi kikubwa ili kukidhi mahitaji ya misaada ya dharura, misaada ya kibinadamu, msaada wa maisha na uingiliaji kati mkubwa katika afya ya umma na ulinzi wa mazingira. " alisema.

Kenya inatarajiwa kuwapelekea maafisa wake wa usalama nchini Haiti huku kukiwa na ghasia za magenge ambayo yametikisa mji mkuu wa nchi hiyo ya Caribbean Port-au-Prince kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Imejitolea kutuma wanajeshi 1,000 nchini Haiti, huku Bahamas wakiwa wamejitolea kuwapeleka wanajeshi wake 150 huku Jamaica, Antigua na Barbuda zikiahidi kusaidia.

Chanzo: Bbc