Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto: Tutapanda miti bilioni tano

Ruto Un Baraza Yusalama Ruto: Tutapanda miti bilioni tano

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya imepanga kupanda miti bilioni 5 katika kipindi cha miaka mitano ijayo lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda maeneo yanye ardhi oevu katika nchi hiyo.

Akizungumzia namna ambavyo nchi yake imejipanga katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Rais wa Kenya Wiliam Ruto amesema mpango huo utawezesha kurejesha maeneo yaliyoharibiwa na shughuli za kibadamu na kuathiri mazingira ya nchi hiyo.

Ameongeza kuwa miti hiyo itasaidia pia utunzaji wa maeneo oevu ambayo ni vyanzo vya maji kwa maisha ya Wakenya na shughuli zao kiuchumi.

Rais Ruto amesema nchi hiyo inafurahishwa na hatua za Tanzania katika kilimo ambacho kitaleta uhakika wa chakula kwa wananchi na kwamba wameanza kutekeleza mipango kadhaa kwenye sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku ya mbolea kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live