Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto: Sijaongea na Kenyatta muda mrefu

Rutoopic Data William Ruto na Kenyatta

Tue, 6 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Mteule wa Kenya, Dkt. William Ruto jana amehutubia Taifa hilo ikiwa ni mara ya kwanza baada ya Mahakama nchini humo kumtaja kuwa Mshindi katika kesi ya kupinga matokeo ya Urais iliyokuwa imefunguliwa na Muungano wa Azimio la Umoja ukiongozwa na Mgombea Urais Raila Odinga.

Katika hotuba yake isiyopungua dakika 40, Ruto huku akicheka alisema hajaongea na rafiki yake mpendwa Rais Uhuru Kenyatta kwa miezi mingi lakini atampigia simu hivi karibuni ili wafanye mazungumzo ya kukabidhiana madaraka.

"Nafahamu alifanya bidii sana kwa namna yake lakini Wakenya wamefanya maamuzi ya chaguo lao ambapo hata hivyo hatuna shida na maamuzi yoyote ya kidemokrasia yanayofanywa na Mkenya yoyote," amesema Ruto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: