Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruto, Gachagua wanavyoigawa UDA Kenya

Ruto Gagachuda Ruto, Gachagua wanavyoigawa UDA Kenya

Thu, 30 May 2024 Chanzo: Mwananchi

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kilichomwingiza madarakani Rais William Ruto kimeanza kufukuta kwa migogoro inayofanana na ile iliyotikisa Chama cha Jubilee cha Uhuru Kenyatta inazidi kuongezeka huku viongozi wakuu wakishambuliana.

Katibu Mkuu wa UDA, Cleophas Malala Jumatano, Mei 29 2024, aliimarisha mlipuko wa kisiasa ndani ya chama tawala kwa kuwataka Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen na mwenzake wa Huduma za Umma Moses Kuria wajiuzulu kutokana na madai yao ya kuhusika na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Malala pia alimlenga Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi, na mbunge wa Githunguri Gathoni Wa Muchomba kwa hatua za kinidhamu kwa madai ya kuleta mgawanyiko ndani ya chama.

Mbali na Kahiga na Wa Muchomba, viongozi wengine wanachukuliwa kama washirika wa karibu wa Rais Ruto.

Taarifa yake ya kushangaza ilimfanya ashambuliwe na baadhi ya viongozi ambao sasa wanamtaka ajiuzulu. Viongozi wengine walimtuhumu Malala kwa kuchukua upande mmoja katika mgogoro huo. Taarifa yake ya kushangaza inaonekana kulenga zaidi wanasiasa wanaomuunga mkono Rais Ruto, jambo lililomweka katika kambi ya Naibu Rais Gachagua.

Mzozo wa madaraka

Mzozo wa madaraka unaozidi kuongezeka ndani ya chama unaakisi yale yaliyosababisha kuvunjika kwa Chama cha Jubilee cha Rais Kenyatta, baadhi ya maofisa wa chama waliomtii Kenyatta walikuwa wakitoa taarifa za kuwafokea baadhi ya washirika wa Naibu Rais Ruto wakati wa mvutano wa Jubilee.

"Imenijia habari kuwa baadhi ya mawaziri wamekuwa wakijihusisha na shughuli za kisiasa, kinyume cha sheria inayowataka wasibague kisiasa. Moses Kuria, Waziri wa Huduma za Umma, jukumu lako kuu ni kuwahudumia watu katika wizara yako. Ukipenda kujihusisha na siasa, unakaribishwa kujiuzulu na kujiunga na siasa," amesema Malala.

"Vivyo hivyo, Kipchumba Murkomen, Waziri wa Barabara na Uchukuzi, unapaswa kuzingatia kushughulikia masuala muhimu katika wizara yako, hasa urejeshaji wa barabara zilizoathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni. Wahudumie Wakenya au ujiuzulu na urejee kwenye siasa," amesema katika taarifa iliyotolewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mara tu baada ya kutua kutoka China.

Shambulizi la kisiasa

Kuria amekuwa akimkosoa Naibu Rais Gachagua, ambaye kwa sasa yupo chini ya shambulizi la kisiasa na baadhi ya washirika wa karibu wa Rais Ruto.

Gachagua hivi karibuni aliwatuhumu baadhi ya washirika wa Rais Ruto kwa kuchochea upinzani dhidi yake katika Mlima Kenya.

Ingawa hakutaja majina, alidhaniwa kumaanisha Murkomen na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi.

"Baadhi ya wanasiasa wachache walio karibu na Rais wanataka kuingilia siasa za Mlima Kenya kunipinga. Siasa za Mlima Kenya ni ngumu sana na tunachokichukia ni usaliti. Kama Mlima Kenya, hatujawahi kuingilia siasa za Bonde la Ufa na tunastahili kuheshimiwa," amesema Gachagua.

Jumatano, Murkomen na Kuria walipuuza madai ya Malala.

Malala pia alimshutumu Gavana Kahiga, Sudi na Wa Muchomba kwa kudhoofisha umoja wa chama wakati akitishia hatua za kinidhamu.

Kahiga amekuwa mmoja wa watetezi wakali zaidi wa Gachagua katika migogoro inayoendelea huku Wamuchomba akiwa mkosoaji wa utawala wa Rais Ruto kutokana na ushuru mkubwa.

Sudi, Jumatano alijaribu kumdharau Malala kwa kumuelezea kama "mjumbe wa Kaunti aliyeinuliwa," huku akijaribu kumfananisha na Katibu Mkuu wa zamani wa Jubilee Raphael Tuju.

Tuju alikuwa maarufu kwa kuandika taarifa kali dhidi ya Ruto alipokuwa Naibu Rais wakati wa mvutano wao na Rais Kenyatta katika Chama cha Jubilee.

Kahiga Jumanne aliiambia Nation kuwa Rais Ruto anahatarisha kupoteza uungwaji mkono wa eneo hilo iwapo atamweka pembeni Gachagua katika uendeshaji wa serikali.

Katika kujibu taarifa ya Malala, mkuu wa kaunti ya Nyeri alitoa wito wa kumwondoa Katibu Mkuu wa chama, akisisitiza kuwa Gachagua lazima aheshimiwe.

"Kaimu Malala katika UDA ni kama msumeno wa mraba kwenye shimo la duara. Hatoshi. Nimesema hapo awali na narudia. Lazima tuondoe katika uchaguzi ujao wa UDA," amesema Kahiga.

Mwenyekiti mwanzilishi wa UDA Johnson Muthama, ambaye sasa anatumikia kama mjumbe wa Tume ya Huduma za Bunge (PSC), amesema inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wakijaribu kuvunja chama hicho ambacho baadhi yao walikifanyia kazi kwa bidii kukijenga.

"Utawala wa Kenya Kwanza uliundwa kwa misingi ya umoja wa kitaifa bila hila za kisiasa na Rais William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua na viongozi wengine walikuja pamoja kwa ajili ya kufanikisha hilo," amesema Muthama.

"Kama mmoja wa viongozi waliopigana kwa bidii kuunda Serikali hii, naamini utawala wetu bado ni mchanga sana kuwa na nyufa kubwa na iwapo kuna matatizo ya mwanzo, tutumie mifumo yetu ya ndani kuyaweka sawa bila kujianika kama ilivyotokea hivi karibuni."

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ambaye amekuwa na mvutano na Gachagua, alijiunga na orodha inayokua ya viongozi wa UDA wanaopinga mtindo wa uongozi wa naibu huyo wa rais.

Gavana Sakaja alimwambia Gachagua aache kumkosoa Rais. Alimtuhumu kwa kuwatisha viongozi wengine katika chama cha UDA.

"Huwezi kuwaburuza watu kwa miaka miwili na kuanza kulia mara tu baada ya kutajwa kwa wiki moja," amesema Sakaja.

Heshimu urais

Lakini Katibu wa Uratibu wa UDA Vincent Musyoka na Mbunge wa Nyaribari Chache Zaheer Jhanda waliwataka viongozi wanaojihusisha na vita vya makundi kuacha na kuheshimu urais.

Wawili hao walisema vita katika Jubilee vilianza kwa njia hiyo hiyo na kusababisha maafa ya kisiasa.

Walisema ni wakati wa Rais kuwaita viongozi wa UDA kwa mpangilio ili kumaliza migogoro hiyo.

Zaheer aliwaambia wanasiasa wa UDA waache kumshambulia Gachagua na badala yake waisaidie urais kutekeleza kwa ajili ya wananchi.

"Ninashangazwa na jinsi baadhi ya wanachama wa UDA wanaweza kumtusi Naibu Rais. Watu wanapaswa kuheshimu ofisi hiyo," amesema.

Chanzo: Mwananchi