Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rushwa yaiondoa kampuni ya Kenya kwenye miradi ya Benki ya Dunia

World Pic Kenya Rushwa yaiondoa kampuni ya Kenya kwenye miradi ya Benki ya Dunia

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Dunia, imelazimika kuifuta Kampuni ya masula ya ushauri ya Kenya inayotekeleza miradi kadhaa ya mamilioni ndani ya Serikali kwa madai ya rushwa.

Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo inaeleza kuwa Kampuni hiyo ya Development Professional Group (ADP), ilikutwa na hatia ya kuhusika katika vitendo vya rushwa mara baada ya kufanyiwa ukaguzi na kitengo cha rushwa cha Benki hiyo.

"Kampuni hii imehusika katika vitendo vya rushwa kwenye miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na Benki ya Dunia ambayo ilikuwa ikitekelezwa nchini Somalia" Imesema taarifa hiyo.

ADP haitatakiwa kushiriki au kujihusisha kwa namna yoyote ile katika miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kipindi cha miezi 21.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live