Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rushwa ya ngono yawaponza wahadhiri

Wahadhiri Morocco Vitendo vya Rushwa ya ngono vimekithiri sana nchini Morocco

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: Mtanzania

Wahadhiri wanne wa vyuo vikuu nchini Moroccco wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kuwaomba rushwa ya ngono wanafunzi wa kike.

Wasomi hao, ambao sasa wanashitakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia, wamejikuta hatiani baada ya kuomba ‘huduma’ hiyo kwa minajili ya kuwapa wanafunzi alama nzuri kwenye mitihani yao.

Ukiacha hao wanne, leo alitarajiwa kufikishwa kizimbani mhadhiri mwingine kwa makosa ya aina hiyo.

Hata hivyo, hiyo inaweza isishangaze kutokana na histori ya vyuo vikuu vya Morocco katika miaka ya hivi karibuni.

Vyuo Vikuu nchini Morocco vimekuwa vikiripotiwa kuwa na utamaduni wa wahadhiri wake kutaka rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike.

Chanzo: Mtanzania