Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruksa kuvaa "Min Skirt" - Mahakama Uganda

949eda6fe41f6c27 Ruksa kuvaa "Min Skirt" - Mahakama Uganda

Wed, 18 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mahakama nchini Uganda imetengua marufuku iliyowekwa kuzuia uvaaji wa sketi fupi. Sheria hiyo ambayo ilipitishwa mwaka 2014, ilikuwa inanuia kuzuia usambazaji wa picha za ngono mtandaoni ili kuwalinda wanawake na watoto.

Jopo la majaji watano wa Mahakama ya Katiba nchini Uganda, kwa kauli moja waliamua kuwa vifungu vya sheria hiyo vinakiuka katibaMajaji hao walisema hakutakuwa na madhara yoyote kwa wanawake na wasichana kuvalia mavazi yanayoonyesha uchiMahakama nchini Uganda imefuta sheria iliyokuwa imepiga marufuku wanawake na wasichana nchini humo kuvaa nguo fupi kufuatia shinikizo la wanaharakati.

Sheria hiyo ambayo ilipitishwa mwaka 2014, ilikuwa inanuia kuzuia usambazaji wa picha za ngono mtandaoni ili kuwalinda wanawake na watoto.

Hata hivyo, waliopinga sheria hiyo walihoji kuwa kanunui hiyo ilitumiwa vibaya na kupelekea wanawake waliovalia nguo fupi kushambuliwa mtaani.

Majaji watoa uamuziWakitoa uamuzi wao, jopo la majaji watano wa Mahakama ya Katiba nchini Uganda, kwa kauli moja waliamua kuwa vifungu vya sheria hiyo vinakiuka katiba.

Majaji hao walisema hakutakuwa na madhara yoyote kwa wanawake na wasichana kuvalia mavazi yanayoonyesha uchi.



Maandamano Uganda kupinga sheria ya minisketiBaada ya sheria hiyo maarufu kama 'sheria ya minisketi' kupitishwa, kulikuwa na maandamano makubwa jijini Kampala kupinga wanawake kudhulimiwa mitaani kwa kuvalia nguo fupi.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu walikwenda kortini wakitaka sheria hiyo ifutwe na sasa imetupiliwa mbali.

Mrembo auawa kwa kuvaa longi Katika taarifa nyingine kuhusu mavazi, mrembo mwenye umri wa miaka miaka 17, alipigwa hadi kufa na familia yake nchini India kwa kutofurahishwa na vazi lake la jeans.

Neha Paswan, kutoka jimbo la Uttar Pradesh, anaripotiwa kupigwa vibaya na babu yake akitumia fimbo kufuatia majibizano kuhusu mtindo wake wa mavazi.

Mama yake Neha, Shakuntala Devi Paswan alisema vurugu ilianza baada ya mwanawe kuvaa suruali ya jeans kufanya ibada zake za maombi.

"Alikuwa amefunga siku nzima kwendana na dini. Wakati wa jioni, akavaa suruali ya jeans na juu akawa na top au aina ya fulana kufanya ibada zake. Wakati babu na bibi yake walipinga mavazi yake, Neha alijibu kwamba jeans zilitengenezwa kwa ajili ya watu kuvaa," alieleza mama huyo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke