Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rubani alazimika kutua baada ya kuona nyoka kwenye kiti chake

Rubani Alazimika Kutua Baada Ya Kuona Nyoka Kwenye Kiti Chake Rubani alazimika kutua baada ya kuona nyoka kwenye kiti chake

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Rubani wa Afrika Kusini anapongezwa kwa kufanikiwa kutua kwa dharura baada ya kuona nyoka aina ya fira ‘Capa cobra’ akiwa amejikunja chini ya kiti chake, ripoti ya vyombo vya habari nchini humo yasema.

Rudolph Erasmus alikuwa akisafirisha abiria wanne kutoka Cape Town kuelekea mji wa kaskazini wa Nelspruit Jumatatu asubuhi lakini alilazimika kukatiza safari baada ya kuhisi kitu cha baridi kwenye mwili wake, aliambia tovuti ya habari ya Times Live.

"Nilipogeuka kushoto kwangu na kutazama chini, niliona nyoka wa aina ya fira ‘Cape’ [cobra] akirudisha kichwa chake chini ya kiti changu," alinukuliwa akisema.

Kuumwa na nyoka aina ya Cape cobra kunaweza kumuua mtu ndani ya dakika 30.

Kamishna wa usafiri wa anga wa Afrika Kusini amemsifu Bw Erasmus kama shujaa, ripoti za tovuti ya news24.

"Rubani hodari ambaye ameokoa maisha ya wote waliokuwa ndani ya ndege," Poppy Khosa alinukuliwa akisema.

Rubani huyo alisema hakuwa na uhakika ikiwa angewaambia abiria wake baada ya kumwona nyoka huyo wakati wa safari ya ndege.

Alisema hakutaka kusababisha hofu.

"Nilisema tu, 'sikiliza, kuna shida. Nyoka yuko ndani ya ndege. Ninahisi kuwa yuko chini ya kiti changu kwa hivyo itabidi tutue ardhini haraka iwezekanavyo,” alinukuliwa akisema. Alifanikiwa kutua kwa dharura huko Welkom.

Wahandisi walioipokea ndege hiyo hawakumpata nyoka huyo, Bw Erasmus alisema.

Chanzo: Bbc