Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti kutokea chini Afrika Kusini, Rais Ramaphosa kazungumza

Screenshot 2021 07 16 At 16.11.27 660x400.png Ripoti kutokea chini Afrika Kusini, Rais Ramaphosa kazungumza hiki

Fri, 16 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais Cyril Ramaphosa wa South Africa amesema leo kuwa Taasisi za usalama Nchini humo zimewatambua watu kadhaa wanaoshukiwa kuchochea vurugu wiki hii.

Ramaphosa ameyasema hayo alipotembelea Manispaa ya Ethekwini ambayo inajumuisha mji wa bandari wa Durban, moja ya maeneo yaliyoathirika pakubwa katika wiki nzima ya uporaji ambao uliharibu mamia ya maduka na kuwauwa zaidi ya Watu 100.

Rais huyu amesema pia Wanajeshi 25,000 watapelekwa katika maeneo yenye vurugu hivi karibuni na hiyo itakua imeongeza idadi ya Wanajeshi mitaani kutoka 10,000 ambayo tayari wameshaingizwa mitaani.

Ramaphosa amesema waliochochea vurugu hizo wanasakwa na pia utulivu umeanza kurejea kwa sehemu katika mji mkuu wa kibiashara Johannesburg japo maduka mengi bado yamefungwa na operesheni katika bandari za Durban na Richards Bay zinaimarika.

Chanzo: millardayo.com