Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ripoti: Wakimbizi DRC wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu

Wakimbizi Hali Congo Drc.jpeg Ripoti: Wakimbizi DRC wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu

Sun, 18 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanaishi katika kambi zisizo salama kiafya mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mzozo kati ya waasi na jeshi la nchi hiyo.

Shirikka la Habari la Iranpress linaripoti kwamba, watu 135,000 wamekimbia kutoka eneo la Sake katika kipindii cha juma moja lililopita na kuomba hifadhi katika mji wa Goma makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wimbi jipya la wakimbizi limeibuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano mapya kati ya jeshi la nchi hiyo na kuundi la waasi la M23.

Mwezi uliopita wa Januari Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilitangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Serikali ya Jamhurii ya Kidemokrasia ya Congo, ilialika kikosi hicho cha SADC baada ya kusema kuwa haijaridhika na wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao walitakiwa kupambana na waasi wa M23.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikimtuhumu jirani yake Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live