Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Reli kwenda Sudan Kusini kujengwa

C781cbe3469044dbb122190699a841b3 Reli kwenda Sudan Kusini kujengwa

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI inapanga kupanua mtandao wa reli kwenda Sudan Kusini

Waziri wa Fedha, Matia Kasaija amesema fedha zipo kwa ajili ya kupanua mtandao wa njia ya reli nchini humo.

Alisema hayo juzi alipokuwa akikabidhi ofisi kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirka la eli Uganda.

“Reli ni njia nafuu ya usafirishaji hivyo uwekezaji katika reli unatakiwa kupewa kipaumbele hasa kurekebisha reli hadi Tororo na ikiwa fedha zinaruhusu italazimika kuijenga hadi Sudan Kusin kwa sababu ndiyo njia ya usafirishaji wa bei nafuu,” alisema.

Sudan Kusini ni soko muhimu la biashara ya nje ya Uganda ikishika nafasi ya pili baada ya Kenya.

Mwaka jana nchi hiyo ilifanikisha Uganda kupata dola za Marekani milioni 351.5 kutokana na biashara mbalimbali.

Kwa upande wake, Stanley Sendegeya alisema kuna mahitaji wa dola za Marekani bilioni moja kwa ajili ya kufufua mtandao wote a reli ikiwamo ukarabati wa laini na kuboresha kutoka chuma hadi kutuia saruji.

Alisema tayari kuna kazi za ujenzi zilizoidhinishwa kama kutoka Tororo-Gulu kwa paundi milioni 47, Kampala-Malaba kwa dola za Marekani milioni 360 na kwamba makadirio ya gharama za Kampala-Kasese ni dola milioni 500 na dola milioni 100 kwa Gulu-Pakwach.

Katika mipango ya muda mrefu na muda wa kati, shirika hilo lina mpango wa kupanua huduma za usafiri wa abiria kati ya Kampala-Namanve, Kyengera na Port Bell na katika mipango ya miaka mitano linalenga kwenda Jinja na Mityana.

Chanzo: habarileo.co.tz