Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Dunia: Mwanamke wa Nigeria apaka rangi kucha kwa siku tatu

Rekodi Za Dunia: Mwanamke Wa Nigeria Apaka Rangi Kucha Kwa Siku Tatu Rekodi za Dunia: Mwanamke wa Nigeria apaka rangi kucha kwa siku tatu

Fri, 3 May 2024 Chanzo: Bbc

Mwanamke mmoja nchini Nigeria anasema amezipaka rangi zaidi ya kucha 4,000 ndani ya saa 72 katika jaribio la kuvunja rekodi ya dunia.

Akiwa na mswaki mkononi Lisha Dachor,19, alizunguka katika kituo kimoja katika jimbo la Plateau, kaskazini mwa Nigeria, akiwapamba mamia ya watu kwa kupaka kucha zao rangi ya samawati, waridi na zambarau.

Harakati zake za kufanya kazi hiyo kwa siku tatu mfululizo zilifikia kikomo siku ya Jumatano.

Sheria za Rekodi ya Dunia ya Guinness (GWR) zinasema kwamba ili lengo lake liweze kutimia Bi Dackor ni sharti apake rangi kucha 60 kwa saa.

Sasa anasubiri GWR kukagua jaribio lake baada ya kuwasilisha ushahidi wake.Bi Dachor alisema alianza changamoto hii ili kubadilisha simulizi kuhusu akina mama vijana kama yeye.

"Nataka kuwapa watu matumaini, haswa akina mama wasio na waume kwa sababu watu wengi hawafikirii kuwa tuna chochote cha kutoa," aliambia BBC.

Fundi huyo wa kucha amekuwa akifanya kazi kitaaluma kwa takriban miaka mitatu na anasema anataka pia kuwaweka wanawake kutoka kaskazini mwa Nigeria katika ramani.

Bi Dachor anasema pia anatumai jaribio lake la rekodi litaweka Plateau, jimbo lake la nyumbani, kwenye ramani ya dunia.

Plateau ni eneo la kaskazini mwa Nigeria lenye Waislamu wengi ambalo linashikana na eneo la Wakristo wengi wa kusini na jamii nyingi uwa zimechanganyika.

Eneo hilo limekabiliana na miongo kadhaa ya ukosefu wa usalama na migogoro kati ya makabila tofauti na makundi ya kidini, ambayo yameshuhudia maelfu ya watu wakiuawa.

Chanzo: Bbc