Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Kenya yaondoa marufuku ya kutoka nje

Video Archive
Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameondoa marufuku ya kutotoka nje kuanzia majira ya jioni hadi Alfajiri nchini humo ambayo iliwekwa Machi 27, 2020.

Ametoa tangazo hilo wakati akihutubia katika siku ya Mashujaa iliyofanyika kitaifa katika mji wa Kirinyaga, na kusema kuwa amefikia maamuzi ya kuondoa marufuku hiyo kufuatia kupungua kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini humo.

"Maambukizi yamepungua kwa kasi sana kwa muda wa wiki mbili sasa, na hadi sasa watu waliorekodia kuwa na ugonjwa huu ni chini ya asilimia 5"

"Hivyo ninaifuta rasmi marufuku hii ambayo ilikuwa ikikataza watu kutoka nje kuanzia jioni, kwasasa amri hii imefutwa!" Amesema Rais Kenyatta.

Mbali na hilo, Rais Kenyatta amesema kuwa jumla ya vijana milioni 5 tayari wameshapatiwa chanjo ya Corona kati ya vijana milioni 10 wa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live