Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni mwanachama wake wa saba na kupanua eneo la jumuiya hiyo ya kibiashara huku ikiwezesha ufikiaji wa Bahari ya Atlantiki na kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wazungumzaji wa Kifaransa katika kile kilichoanza kama klabu ya koloni za zamani za Uingereza.
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameidhinisha kuingizwa kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika umoja huo katika mkutano wa kilele siku ya Jumanne, lakini ingawa imekuwa mwanachama rasmi, hakuna mengi yanayoweza kubadilika mara moja.
Wabunge wa Kongo bado wanapaswa kuidhinisha sheria na kanuni za EAC kabla ya kuanza kutumika.
Raia wa Kongo wanaotaka kutembelea nchi nyingine wanachama - Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda - bila visa wanaweza kuhitaji kusubiri kwa muda mrefu zaidi kwa sababu ushirikiano kamili katika EAC unaweza kuchukua miezi au hata mwaka.