Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Bobi Wine apitishwa kugombea Urais

A4dbfaa5 9c9b 4862 B8ae E93f23b78058 Rasmi Bobi Wine apitishwa kugombea Urais

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Tume ya Uchaguzi Uganda imempitisha Mbunge wa Kyadondo na Mwanamuziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine kugombea Urais wa Nchi hiyo.Baada ya risiti zake kukaguliwa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Justice Simon Byabakama amesema “Tumethibitisha stakabadhi zilizowasilishwa na mgombea kwamba ametimiza vigezo vyote vya uteuzi.”

Bobi Wine pia alikumbushwa na Tume kwamba mikusanyiko ya umma bado imepigwa marufuku na kwamba kampeni zake zote zitaendeshwa kulingana na miongozo ya Tume ya Uchaguzi.

Bobi amenukuliwa akisema “huu ni mwanzo mzuri kuelekea kuiokomboa Uganda, nimekuja kumsaidia kazi Mzee wangu Museveni ambaye amekaa Ikulu kwa miaka 34 tangu mwaka 1986?

Bobi atachuana na Rais Yoweri Museveni kwenye kuwania Urais wa Uganda kwenye uchaguzi wa mwaka 2021.

UWEZO WA KOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI

Chanzo: millardayo.com