Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramaphosa kuhojiwa kuhusu Zuma leo

SOUTH AFRIKA Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, leo anatarajiwa kufika mbele ya jopo la uchunguzi wa madai ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa Rais wa mtangulizi wake Jacob Zuma.

Jopo hilo lilianzishwa kuchunguza madai hayo kwa kuruhusu familia tajiri ya Gupta kupora rasilimali za serikali Wote wawili Zuma na Gupta wanakanusha makosa yoyote.

Ufisadi huo unakadiriwa kuigharimu Afrika Kusini kiasi cha $ 81bn (£ 58bn) ambazo ni fedha za umma huku ikipoteza fursa nyingi ikiwemo za ajira kwa vijana zenye manufaa kwa taifa zima.

Wakati wa utawala wa Rais Zuma, Ramaphosa likuwa ni naibu Kiongozi wa chama cha ANC, na kuitwa kwake hii leo ni kwaajili ya kukamilisha uchunguzi wa madai yanayomkabili Zuma kwa kueleza kile ambacho chama cha ANC kinafahamu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live