Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramaphosa ayataka mashirika kununua chanjo ya COVID-19 Afrika

Chanjoopicc Data Ramaphosa ayataka mashirika kununua chanjo ya COVID-19 Afrika

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameyataka mashirika ya kimataifa na mashirika ya wafadhili kununua chanjo za Covid kutoka kwa wazalishaji wa Kiafrika.

Rais Ramaphosa amesema hili "litahakikisha uwezo unaoendelea katika bara unadumishwa", alipokuwa akizungumza na mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu Covid , Alhamisi.

“Mashirika ya kimataifa ambayo yamechangiwa fedha nyingi kwa ajili ya kununua na kupata chanjo kwa nchi zinazoendelea kiuchumi, hayanunui chanjo kutoka kwa watengenezaji chanjo barani Afrika, hata kwa zile chanjo ambazo zimewekwa kwa nchi za Afrika,” alisema.

Taarifa hii inakuja wakati mtengenezaji wa chanjo nchini Afrika Kusini anatoa angalizo la kusimamisha uzalishaji wa chanjo kwa kukosa watu wanaoagiza.

Aspen Pharmacare hivi majuzi ilisema kwamba inaweza kulazimika kusitisha uzalishaji katika kiwanda chake cha Afrika Kusini baada ya kukumbwa na uhitaji mdogo.

Kampuni ilijadili mkataba wa kutoa leseni mwezi Novemba ili kufunga na kuuza chanjo ya Johnson & Johnson ili kusambazwa barani Afrika.

Ilionekana kama nyongeza ya uzalishaji na usambazaji wa chanjo barani Afrika.

Lakini, bara bado lina kiwango cha chini cha chanjo hata wakati linakabiliwa na wimbi jipya la virusi.

Kati ya Waafrika sita, mmoja ndio amepata dozi mbili za chanjo ya virusi vya corona, huku wengi wakisita kuchapwa.

Siku ya Alhamisi, Bw Ramaphosa alisema nchi yake bado inatetea msamaha wa haki miliki ili kuboresha ufikiaji wa kimataifa wa chanjo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live