Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramaphosa awaonya wafanyakazi wanaogoma baada ya maandamano

Ramaphosa Awaonya Wafanyakazi Wanaogoma Baada Ya Maandamano Ramaphosa awaonya wafanyakazi wanaogoma baada ya maandamano

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Rais Cyril Ramaphosa anasema ana wasiwasi kuhusu mgomo unaoendelea wa mishahara wa wafanyikazi wa umma ambao unaathiri huduma muhimu nchini.

Mgomo wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyakazi wa Elimu, Afya na Washirika (Nehawu) ulianza Jumatatu, huku wafanyikazi wakidai nyongeza ya 10% ya mishahara baada ya kukataa nyongeza ya 3% ya serikali.

Takriban watu wanne wamefariki huku wafanyakazi hao wakiripotiwa kuwazuia wagonjwa kuingia katika hospitali na kliniki nyingi nchini, Waziri wa Afya Joe Phaahla alisema.

Rais alisema siku ya Alhamisi kwamba ingawa wafanyikazi wana haki ya kugoma, vitendo vya ghasia havitavumiliwa.

“Sote tuna wasiwasi kuhusu hali ya vurugu ya mgomo unaoendelea. Wafanyakazi katika nchi yetu wana haki ya uhuru wa kujumuika na kugoma. Lakini haki hiyo si kamilifu," Rais Ramaphosa alisema.

Alisema kuwa kanuni ya "hakuna kazi, hakuna malipo" inapaswa kutumika kwa wafanyikazi wa huduma muhimu wanaogoma

Chanzo: Bbc