Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramaphosa atuma jeshi kupambana na migodi haramu

Migodi Haramu Afrika Kusini.jpeg Ramaphosa atuma jeshi kupambana na migodi haramu

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameidhinisha kutumwa wanajeshi 3,300 wa Jeshi la Ulinzi la Taifa la Afrika Kusini (SANDF) ili kushirikiana na polisi kuzuia na kupambana na uhalifu na kudumisha amani na utulivu katika maeneo ya migodi nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Afrika Kusini imesema: SANDF, ikifanya kazi kwa kushirikiana na polisi, itaendesha operesheni kali dhidi ya uhalifu unaofanywa na wachimbaji haramu wa madini katika majimbo yote ya nchi hiyo, operesheni ambayo inatarajiwa kumalizika Aprili 28, 2024.

Gharama zilizokadiriwa kufanikisha opereshenei hiyo ni zaidi ya randi milioni 492 (kama dola za Kimarekani milioni 27). Kutumwa kikosi cha Jeshi la Taifa SANDF kunakuja kutokana na kuongezeka sana uchimbaji haramu wa madini na uhalifu wa kikatili katika kona mbalimbali za Afrika Kusini.

Wiki iliyopita pia kuliripotia habari ya kugunduliwa makumi ya maiti waliosadikiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa migodi. Polisi ya Afrika Kusini ilianzia uchunguzi kuhusu tukio hilo ambalo liliripotiwa kutokea kwenye mji wa Krugersdorp, magharibi mwa jiji la Johannesburg.

Jeshi la Afrika Kusini limetumwa kusaidia polisi kupambana na uhalifu na wachimbaji haramu wa madini

Msemaji wa Polisi ya Afrika Kusini, Brenda Muridili alisema kuwa, waliopoa maiti 19 kwenye mgodi binafsi katika mji huo Jumatano iliyopita, huku miili mingine miwili ikigunduliwa siku ya pili yake.

Jeshi la Polisi nchini humo lilisema kuwa, yumkini wachimba migodi hao waliuawa sehemu tofauti, kisha miili yao ikapelekwa karibu na mgodi huo binafsi mjini Krugersdorp.

Kesi hiyo ni sehemu ya wimbi la matukio ya kihalifu yanayohusishwa na uchimbaji madini kinyume cha sheria katika mji wa Krugersdorp, ulioko magharibi mwa mji wa Johannesburg ambao ni makao makuu ya mkoa wa Gauteng.

Mwezi Julai mwaka huu pia, wanawake wanane waliokuwa katika timu ya kutengeneza filamu walibakwa na mali zao kuporwa katika mgodi uliotelekezwa wa eneo la Krugersdorp.

Kutokana na hali ngumu ya maisha, akthari ya wananchi wa Afrika Kusini wa maeneo yenye utajiri wa madini wamekuwa wakichimba migodi ambayo si salama, kinyume cha sheria.

Wadadisi wa mambo wanavilaumu vyombo vya dola nchini humo, kwa kushindwa kudhibiti shughuli hizo za uchimbaji madini kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live