Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramaphosa ataka amani ya kudumu Palestina

Ramaphosa Anasema Mkutano Wa BRICS Utakuwa Ana Kwa Ana Ramaphosa ataka amani ya kudumu Palestina

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini sanjari na kupongeza usitishaji vita wa muda kwa misingi ya ubinadamu huko Gaza, ametoa mwito wa kufanyika jitihada zaidi za kutafuta amani ya kudumu na endelevu katika mgogoro wa miongo kadhaa baina ya Palestina na utawala haramu wa Israel.

Ramaphosa ametoa mwito huo katika taarifa na kueleza kuwa: Usitishaji huu, ambao kwa masikitiko unaashiria uwezekano wa kuendelea mgogoro kwa wakati fulani, unapasa kuambatana na juhudi zisizoisha za kutafuta azimio la kudumu la kisiasa, kwa mgogoro huu wa miongo kadhaa Mashariki ya Kati.

Rais wa Afrika Kusini amesema anatumai makubaliano hayo ya kusitisha vita kwa muda wa siku nne utaimarisha juhudi za kuhitimisha kikamilifu mgogoro wa sasa katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya Ramaphosa imekuja siku moja baada ya Bunge la Afrika Kusini Jumanne kupiga kura ya kufunga ubalozi wa utawala huo ghasibu, kusimamisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo na kumfukuza balozi wa Kizayuni nchini humo. Waafrika Kusini katika maandamano ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina

Kabla ya hapo, Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni ilikuwa imetangaza kuwa, imemwita nyumbani balozi wake mjini Pretoria kwa ajili ya mashauriano kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya viongozi wa Afrika Kusini.

Aidha katika kukabiliana na jinai hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, Pretoria imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kumkamata Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu kwa tuhuma za mauaji ya halaiki.

Makumi ya maelfu ya Waafrika Kusini wamekuwa wakifanya maandamano ya kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za Israel hususan mauaji ya kimbari ya watoto wadogo na wanawake huko Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live