Rais wa Afrika Kusini ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake huko Hague Uholanzi ichunguze haraka iwezekanavyo jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza.
Rais Cyril Ramaphosa mapema wiki hii alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa nyaraka zinazohusiana na jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza zimekabidhiwa kwa mahakama ya ICC na inasubiriwa kutolewa agizo ili uchunguzi uanze mara moja.
Rais wa Afrika Kusini ametaja kuendelea mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
UIsrael inafanya mauaji makubwa ya kikatili Ukanda wa Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya raia wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina tangu Oktoba 7 mwaka huu kwa himaya na uungaji mkono wa pande zote za nchi za Magharibi.
Hadi sasa Wapalestina elfu 19,667 ambao aghalabu yao ni wanawake na watoto wameuliwa shahidi na wengine elfu 52,586 kujeruhiwa tangu utawala wa Kizayuni uanzishe mashambulizi ya kikatili dhidi ya Ukanda wa Gaza.