Fri, 2 Dec 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Vyanzo mbalimbali ikiwemo Bloomberg vimeripoti kuwa Rais Cyril Ramaphosa yuko kwenye mashauriano na watu wake wa karibu juu ya uamuzi huo kutokana na ripoti ya uchunguzi kuonesha alivunja Katiba ya Nchi.
Ramaphosa anakabiliwa na kashfa ya kuficha zaidi ya Tsh. Bilioni 9 kwenye shamba lake, fedha hizo ziliibwa na wafanyakazi wake ambao inadaiwa aliwateka ili kuwanyamazisha.
Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa, Arthur Fraser alimfungulia kesi Rais Ramaphosa Juni 2022 juu ya kuficha pesa shambani. Chama Tawala (ANC) kimetangaza kukutana Desemba 16, 2022 kujadili kashfa hiyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live