Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramaphosa: Afrika Kusini haitakuwa huru mpaka Palestina ikombolewe

Rais Ramaphosa Adaiwa Kutohusika Na Wizi Wa Fedha Ramaphosa: Afrika Kusini haitakuwa huru mpaka Palestina ikombolewe

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kukwa, idadi kubwa ya watu wa nchi yake, pamoja na serikali na chama tawala cha African National Congress (ANC) wanaunga mkono harakati za wananchi wa Palestina kupigania uhuru.

Rais Ramaphosa amesema hayo mbele ya mashabiki wa soka kwenye mechi ya kukusanya fedha kwa ajili ya Palestina iliyofanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini na kusisitiza kwa kuksema: "Tunafuata nyayo za Nelson Mandela ambaye alituambia na kutufundisha kwamba... uhuru wetu hautakamilika hadi uhuru wa Wapalestina utakapopatikana."

Vilevile amesema kukwa, Afrika Kusini haiwezi kuhesabiwa kuwa ni nchi huru hadi pale Palestina itakapopata uhuru wake kamili.

Rais Ramaphosa amesema hayo huku akishangiriwa kwa shangwe kubwa na mashabiki wa soka kwenye Uwanja wa Athlone mjini Cape Town na kusisitiza kwamba: "Kwa hivyo sisi pia hatuko huru kabisa hadi Wapalestina wawe huru... tutasimama na tutapambana bega kwa bega nao na ndiyo maana tulikwenda Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuishitaki Israel." Afrika Kusini imesimama imara kulitetea taifa la Palestina

Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa mechi ya timu ya taifa ya Palestina mjini Cape Town kwa ajili ya mchezo wa Soka wa kukusanya fedha za kuwasaidia Wapalestina wanaoshambuliwa kinyama na utawala wa Kizayuni. Mechi hiyo ilimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila la Afrika Kusini dhidi ya wenyeji wao, timu ya taifa ya Palestina.

Mechi inayofuata ya mshikamano na Wapalestina ambayo imepewa jina la "Kombe la Uhuru," itafanyika katika uwanja huo huo wa mpira tarehe 18 mwezi huu wa Februari.

Mwishoni mwa 2023, Afrika Kusini ilifungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya ICJ huko The Hague, Uholanzi, ikiushutumu uutawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina tangu mwaka 1948. Mahaka hiyo ilitoa hukumu kwa manufaa ya Wapalestina na Afrika Kusini dhidi ya Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live