Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa zamani wa Madagascar afariki dunia

Screenshot 2021 03 29 At 13.51.33 660x400.png Rais wa zamani wa Madagascar afariki dunia

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina ametangaza kifo cha Rais wa zamani Admirali Didier Ignace Ratsiraka, aliyefariki Mach 28, 2021 katika Hospitali ya Jeshi ya Soavinandriana.

Ratsiraka amefariki akiwa na miaka 84, baada ya kulazwa tangu Machi 22. Rais Rajoelina amesema wananchi wa Taifa hilo wamepoteza mzalendo.

Ratsiraka aliongoza Madagascar kwa mihula miwili 1975 hadi 1993 na mwaka 1997 hadi 2002. Aliposhindwa Uchaguzi Mkuu wa 2002 alienda Ufaransa.

Akiwa Ufaransa mwaka 2003, alihukumiwa bila kuwa mahakamani baada ya kukutwa na kosa la ufisadi. Baadaye, Rais Rajoelina alimuachia huru.

Chanzo: millardayo.com