Rais wa zamani wa Ivory Coast Henri Konan Bedie, mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotawala siasa katika taifa hilo la Afrika magharibi, amefariki akiwa na umri wa miaka 89, ndugu yake wa karibu ameliambia shirika la habari la Reuters Jumanne.
Rais wa zamani wa Ivory Coast Henri Konan Bedie, mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotawala siasa katika taifa hilo la Afrika magharibi, amefariki akiwa na umri wa miaka 89, ndugu yake wa karibu ameliambia shirika la habari la Reuters Jumanne. Bedie alihudumu kama rais kuanzia mwaka 1993 hadi alipoondolewa madarakani mwaka 1999 na baadaye akagombea urais ambao alishindwa dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu Rais Alassane Ouattara katika uchaguzi wa 2020, alipokuwa na umri wa miaka 86.