Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa zamani wa Afrika Kusini afariki akiwa na miaka 85

FW CLERK Rais wa zamani wa Afrika Kusini afariki akiwa na umri wa miaka 85

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekua Rais wa zamani wa Afrika Kusini na mzungu wa mwisho kuiongoza nchi hiyo, FW de Klerk amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.

Bw de Klerk, ambaye pia alikuwa mhusika mkuu katika kipindi cha mpito cha taifa kuelekea demokrasia, alikuwa akiugua saratani mwaka huu, taarifa ya msemaji imeeleza.

Bw de Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994.

Mwaka 1990 alitangaza kumwachilia huru kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela, na kuruhusu kura za vyama vingi mwaka 1994.

Taarifa kutoka kwa wakfu wa Rais wa zamani wa FW de Klerk siku ya Alhamisi asubuhi imesomeka: "Rais wa zamani FW de Klerk amefariki kwa amani nyumbani kwake Fresnaye (Cape Town) mapema leo asubuhi kufuatia mapambano yake dhidi ya saratani ya mesothelioma."

Taasisi hiyo ilikuwa imetangaza utambuzi huo - saratani inayoathiri utando wa mapafu - mwezi Juni mwaka huu.

FW de Klerk alikuwa amechukua nafasi ya PW Botha kama mkuu wa Chama cha Kitaifa mnamo Februari 1989 na mwaka uliofuata akatangaza kuwa anaondoa marufuku ya vyama vilivyojumuisha chama cha Mandela cha African National Congress (ANC).

Matendo yake yalisaidia kukomesha enzi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, na akawa mmoja wa naibu marais wawili wa nchi hiyo baada ya uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1994 ambao ulishuhudia Bw Mandela akiwa rais.

Alishiriki Tuzo ya Amani ya Nobel na Bw Mandela mnamo 1993.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live