Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa zamani Tunisia acharuka sakata la kufutwa kwa uislamu

Rais Zamani Tu Niasia Rais wa zamani Tunisia acharuka sakata la kufutwa kwa uislamu

Mon, 27 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Al Marzouq amesema anawatolea wito wananchi wa Tunisia kususia kura hiyo tarajiwa ya maoni kuhusu katiba mpya ya Tunisia. Moncef al Marzouq alikuwa Rais wa Tunisia kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.

Kabla ya al Marzouq kutoa wito huo, Rashed al Ghanouchi Spika wa Bunge la Tunisia aliyefukuzwa ambaye ni mkuu wa Chama cha Kiislamu cha nchini humo cha An Nahadhah pia alitoa wito wa kususiwa kura hiyo tarajiwa ya maoni.

Rais Kais Saeid wa Tunisia ametangaza kuwa, kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo itafanyika Julai 25 mwaka huu.

Rais wa Tunisia Juni 25 mwaka jana alichukua madaraka ya Tunisia kwa kutekeleza hatua kadhaa za aina yake ambapo alisimamisha Bunge na kumfuta kazi spika wake, pamoja na waziri mkuu wa serikali, na kuchukua udhibiti wa mambo yote ya nchi.

Hatua ya Rais Saed ya kuifuta kazi serikali ilisababisha mkwamo mkubwa wa kisiasa nchini humo ulioibua malalamiko na upinzani wa vyama na mirengo mbalimbali ya kisiasa khususan chama cha An Nahadhah.

Wapinzani wa Rais Kais Saeid wanamtuhumu kwa kufanya mapinduzi dhidi ya mafanikio ya kidemorasia yaliyopatikana katika vuguvugu la mapambano ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Rais Zainul Abidin bin Ali, hata hivyo Kais Saeid anasema, hatua alizochukua ni halali na kwamba kulikuwa na udharura wa kufanya hivyo ili kuinusuru Tunisia katika dimbwi la mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live