Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa zamani Sierra Leone aruhusiwa kusafiri nje ya nchi

Sierra Leon Aruhusiwa Rais wa zamani Sierra Leone aruhusiwa kusafiri nje ya nchi

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu mjini Freetown Sierra Leon imempatia kibali cha kusafiri nje ya nchi kwa sababu za kimatibabu Rais wa zamani wa nchi hiyo Ernest Bai Koroma.

Koroma alituhumiwa kwa makosa ya uhaini na mengine kadhaa kufuatia jaribio lililofeli la mapinduzi la mwezi Novemba mwaka jana lililosababisha vifo vya watu 20 huko Sierra Leone.

Mahakama Kuu ya Freetown ilitoa uamuzi kuwa Koroma hawezi kukaa Nigeria kwa zaidi ya miezi mitatu na kwamba anapasa kurejea Sierra Leone ili kufika mahakama tarehe Machi mwaka huu.

Wakili mkuu wa Koroma, Joseph Fitzgerald Kamara, alizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo,ambapo alisema: Amri ya kutozungumza imetolewa, na hivyo hakuweza kutoa maoni yake kuhusu yaliyomo katika uamuzi wa mahakama.

Uamuzi huo unakuja huku kukiwa na uvumi kwamba kiongozi huyo wa zamani amekubali kwenda uhamishoni nchini Nigeria iwapo mashtaka dhidi yake yatafutwa. Itakumbukwa kuwa Ernest Bai Koroma alitiwa mbaroni mwanzoni mwa mwezi Januari akituhumiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililofeli.

Katika jaribio hilo la mapinduzi lililoshindwa huko Sierra Leone , watu wenye silaha walivamia kambi ya kijeshi na magereza kadhaa huko Freetown ambapo wafungwa karibu 2,000 waliachiliwa huru. Takriban watu 30, wakiwemo polisi, wanajeshi na mlinzi wa zamani wa Koroma wameshtakiwa kwa madai ya kuhusika katika uasi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live